Header

“Sanchez bado ni Mali ya Arsenal”;- Mourinho

Kocha mkuu wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kuwa hakuna Makubaliano baina ya Klabu yake pamoja na Arsenal juu ya uhamisho wa Alexis Sanchez licha ya kukiri kuwa wapo katika mbio za kumuwania katika kipindi hiki cha Usajili.

Mourinho amezungumza na Waandishi wa habari baada ya Mchezo dhidi ya Stoke City uliomalizika kwa United kushinda 3-0. Kocha huyo amesema anachofahamu Mchezaji huyo ni wa Arsenal wanaojua kuhusu kuondoka kwake ni Kocha Wenger na Uongozi wa Arsenal.

“Ni Mchezaji wa Arsenal anaweza kuondoka au kubaki kama ataondoka Arsenal tutakuwa na nafasi kumpata ingawa kwa Mchezaji mkubwa kama yeye Vilabu vingi vikubwa vinamtaka na hakuna anayejua zaidi yake yeye (Sanchez) kocha wake Arsene Wenger pamoja na Uongozi wake”. Alisema Mourinho

Sanchez amekuwa akihusishwa na kujiunga na Mashetani wekundu katika Dirisha dogo la Usajili kwa ada ambayo inatajwa kuwa Paundi Milioni 40 pamoja na Mchezaji Mikhitaryan kujiunga na Arsenal.

Nyota huyo wa Chile anamaliza Mkataba wake Mwishoni mwa Msimu huu ambapo anaweza kujiunga na Klabu yoyote itakayomuhitaji bure.

 

 

Comments

comments

You may also like ...