Header

Makala: Njia Tatu Wasanii wa Bongo wanavyopiga Pesa kupitia Mitandao ya kijamii

Likiwa ni Zao la vita baridi iliyoigawanya dunia katika makundi mawili hasimu baada ya vita ya pili ya dunia, Internet imewezesha kuzaliwa kwa mitandao ya kijamii. Kwa mujibu za takwimu kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania yaani TCRA,zinasema kuwa mpaka kufikia disemba 2016 watanzania Zaidi ya milioni 20 wamekua wakitumia mtandao wa internet. Hii ikiamaanisha karibu ya nusu ya watanzania wote hutumia huduma hii ya internet.

Na inakadiriwa kuwa zaidi ya watanzaania milioni 16 wanatumia mitandao ya kijamii, na mitandao ya kijamii iliyo maarufu  ni kama vile Instagram,Facebook ,Twitter na Jamii forum kwa kuzitaja kwa uchache.

Wasanii na watu maarufu wamekua miongoni mwa watumiaji maarufu wa mitandao hii ya kijamii nchini Tanzania.

Jumbe mabilmbali zimekua zikipamba kurasa mbalimbali katika mitandao ya kijamii ya wasanii,zikiwa zimesheheni elimu,kejeli,Mipasho,Onyo,tambo,taarifa,michango na hata saa nyingine maneno ya kuudhi. Katika siku za hivi karibuni tumeshuhdia matangazo mengi ya kibiashara kwenye kurasa za wasanii wa muziki wa kizazi kipya ,bongo movie na hata watu maarufu.

Hii ikanilazimu kulitafakari na kuamua kufanya utafiti kidogo ambao uliohusisha  kuhoji baadhi ya marafiki zangu wasanii na kupitia baadhi ya kumbukumbu za mahojiano. Inaoekana ni mbinu mpya inayotumiwa na wasanii kujiingizia kipato kikubwa.

Hizi ni njia tatu ambazo wasanii huzitumia kupiga pesa kupitia mitandao ya kijamii,Njia zipo nyingi lakini kwa leo tuziangalie hizi tatu ingawa hakuna kiasi halisi cha pesa waingizapo kupitia mitandao ya kijamii hutajwa,kutokana na usiri  na mamlaka husika haijatilia mkazo katika kudai ama kufuatilia biashara hii.

  • Kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali wazitoazo.

Kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia wasanii wengi wakijikita katika suala zima la ujasiriamali, ambapo kurasa zao kupitia mitandao ya kijamii kama vile Instagram, imekua ikitumika kutangaza biashara na huduma mbalimbali zitolewazo na wasanii wenyewe.

Msanii kama Alikiba  ameonekana kutumia ukurasa wake wa Instagram katika kutangaza kofia na tsheti zake za “King Kiba” na pia Jux nae  amekua akitumia kurasa zake kutangaza bidhaa zake za “African boy”

Naye Diamond Platinumz hayuko nyuma katika hili, amekua akiweka bidhaa  zake kama vile “Diamond Karanga” “Chibu Perfume” na amekua akiendesha kampeni mbalimbali za mauzo ya bidhaa zake kama kampeni ya “tukutane sheli” amabayo ina lengo la kuhamasisha mauzo ya  bidhaa yake ya karanga. Hii imechangia kununuliwa kwa wingi kwa bidhaa hii sokoni,nilifanya utafti wangu mdogo kwa baadhi ya wauzaji wa bidhaa hii,wakanambia  sasa hivi inanunuliwa sana kutokana na kampeni hiyo ya mauzo huusisha bahati nasibu ya vitu mbalimbali kama gari na pikipiki. Kwa mafanikio haya huwezi yatenganisha na ukurasa wa Diamond Platinumz wa Instagram.

Tukiachana na wasanii wa bongo flavor ,wasanii wa bongo movie nao hawako nyuma kwenye hili,Msanii wolper amekua akitumia kurasa wake wa instagram kulitangaza duka lake la nguo za kushona lijukanalo kama “House of Stylish”. Na siku za hivi karibuni naona Aunt Ezekiel kupitia kurasa wake wa instagram akitangaza huduma yake mpya ya kutoa huduma ya vilevi katika shughuli mbalimbali kupitia “Cookie Liquor Store”

Msanii shilole au kwa sasa Mrs Ashrafu, amekua akiweka matangazo ya huduma yake aliyoianzisha ya chakula iitwayo “shishi food” au mwenyewe hupenda kupaita “unyamwezini empire” na hivi karibuni amesikika akija na bidhaa yake ya Chill ambayo amemuomba Diamond Platinumz amsaidie kuipromote. Nadhani hapa moja ya msaada  Diamond Platinumz anaweza kutoa ni kumsaidia kupost katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii haswa mtandao wa Instagram ambao ana watu wanaomfuata Zaidi ya million nne.

Nyimbo nazo ni miongoni mwa bidhaa wasanii wa bongo fleva wamekua wakizitambulisha kupitia mitandao ya kijamii na kuweka viunganisho vya  “Youtube” na maneno  kama “link in my bio” or “Link in his bio” yamekua maarufu pale msanii anapotoa wimbo au kushirikishwa huyatumia kumuongoza shabiki kuitazama video hiyo au sauti ya wimbo huo kwenye “social sharing network” kama youtube na Itune.

Hii imesadia kupanda kwa idadi ya watazamaji wa video kupitia “Youtube”. Na kwataarifa yako kama hujui, Youtube hulipa wasanii walioweka nyimbo zao katika ukurasa huo, ambapo hulipwa kutokana na factors mbalimbali kama idadi ya watazamaji,watu walivyoipenda na watu waliojiandikisha kupokea taarifa maarufu kama “subscribers” na nyingine nyingi.

Matangazo hayo kupitia Akaunti hizi za wasanii wamekua wakipata mrejesho mzuri kutoka kwa wateja na mashabiki wao . Ushahidi wa awali ni maoni yatolewayo na baadhi ya mashabiki wao kupitia kurasa zao.

  • Kufungua makampuni yanayojihusisha kuuza Nyimbo mtandaoni na kuendesha Akaunti za Youtube.

Hii ni njia nyingine ambapo wasanii na watu wengine maarufu hapa mjini wanapiga pesa, hapa ntawaongelea watu watatu  ambao ni Diamond Platinumz,Michael Mligwa a.k.a Mx Carter na Maxence Melo, ntakuonyesha jinsi wanavyoingiza mkwanja kupitia hizi “online platforms”

Diamond Platinumz, licha ya kuwa mwanamuziki pia ameanzisha “online platform” ijukanayo kama WASAFI.COM ambayo huuza nyimbo zake na za wasanii wengine mtandaoni. Ambapo huuza nyimbo moja kwa shillingi miatatu.Msanii mmoja siwezi mtaja jina lake kwasababu za kimaslahi alinambia alilipwa zaidi ya milioni saba kwa nyimbo yake kuuzwa mtandaoni na kampuni moja ya uuzaji wa mziki mtandaoni . Kwa hali hii huenda diamond anaingiza mkwanja mrefu kupitia wasafi.com, pengine ndo tunaona matunda kama ya NEW WASAFI HEADQUARTER au yale ya MNARANI.

Michael Mligwa a.k.a MX CARTER, one of the coolest bro i ever met, ndo naweza kumuongelea huyu jamaa, ni muanzilishi wa kampuni linalotrend kwa sasa la upigaji picha la SLIDE VISUALS LIMITED, MX anajihusisha pia na kuendesha Akaunti za Youtube za wasanii kama Shetta,Shilole,Msami, Fid Q ,Lady Jay Dee na kipindi flani Baraka De Prince. Mx ndo anahusika kufanya mambo yote malipo kwa wasanii hao ambayo yanahusu mapato ya youtube.

Maxence Melo, huyu ni mwanzilishi wa wa jukwaa la kijamii la Jamii Forum, Max anapiga pesa kutokana na  matangazo ya huduma ya makampuni mbalimbali yaliyopo katika jukwaa .hilo kama  wewe ni mtumiaji mzuri wa mtandao huo,utashuhudia idadi kadhaa ya matangazo ya makampuni makubwa ya simu, serikali na pia matangazo ya vipindi vya television mbalimbali. na pia wana akaunti ya Youtube ambayo nayo huingiza kipato.

 

  • Kuweka matangazo ya makampuni ya kibiashara katika kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Hii ni moja ya njia ambayo huenda inawapa pesa wasanii pengine tukishuhudia wakidrive magari makali na kuishi “uzunguni”. Makampuni makubwa na madogodogo  yamekua yakitumia wasanii wenye wafuasi wengi katika mmitandao ya kijamii katika kutangaza huduma zao.

Mfano ni kampuni kama GSM kupitia GSM malls matangazo yao yamekua yakionekana katika kurasa za wasanii mbalimbali kama ukurasa wa Diamond Platinumz, Ommy Dimpoz na katika kurasa za watangazaji maarufu kama Milard Ayo na Dizzim online.”jamaa anaingiza sana pesa,umeona hayo matangazo yamekua yakimpatia sana fedha  nyingi” alisikika mmoja wa wandani wangu wa taarifa kutoka kwa msanii mmoja mkubwa.

kwenye utafiti wangu usio rasmi makampuni haya hulipa pesa kwanzia shillingi elfu 50000 au kwa makubaliano maalumu. Mwaka 2016 Marehemu “Bikira wa Kisukuma” Mwenyezi Munguamlaze mahala pema peponi.

Akihojiwa katika kipindi cha mkabesa show kilichokuwa kikrushwa pale TV1 alisikika akisema amekuwa akilipwa kuanzia shillingi laki moja kwa Tangazo, alilokuwa akipost katika kurasa wake ambao ulikua maarufu Instagram.

Zaidi ya hayo pia tumeona wasanii wakiwa mabalozi wa makampuni na bidhaa mbalimbali ambapo tumekua tukishuhudia ubalozi wao kupitia mitandao ya kijamii kwa mfano Irene Uwoya amekua balozi wa simu za Itel ,Diamond na Belaire ya Ufararansa.

Natumai msomaji utakua umepata mwanga jinsi gani wasanii na watu maarufu bongo wanavyopiga pesa kupitia mitandao ya kijamii, ingawa sijaweka ni kiasi gani wanaingiza kwa mwaka kutokana na usiri mkubwa uliotanda miongoni mwa wasanii hawa na pia kukosekana kwa kumbukumbu za malipo. Natumaini mamlaka ya mapato TRA wafikilie ,hiki kinaweza kuwa chanzo kipya cha mapato.

kwa maoni na ushauri nicheki kwenye namba +255759623108

Comments

comments

You may also like ...