Header

Rama Dee agonganishwa na muziki wa Kenya

Msanii na Staa wa muziki wa RnB kutoka Tanzania, Rama Dee amegonganishwa uwezo wake na kolabo ya wimbo mpya wa wakali wawili kutoka Kenya, rapa Khaligraph na Timmy T Dat unaokwenda kwa jina ‘KasaYole’.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Rama Dee alipost picha nakili(Screenshot) ya maoni ya shabiki mmoja kutoka Kenya aliyesikiliza wimbo mpya ‘Furaha Yetu’ wa Rama Dee uliomshirikisha rapa Joh Makini na kuweka lawama ya kuwa muziki wa Kenya unaonekana kuwa na tatizo katika ulinganisho wake na wimbo huo wa Rama Dee.

“this Kenya music industry is fucked up..radio stations busy playing fucking Kasayole while we have nice music our here..Nani alituroga?” Shabiki aliyejiita Elius Robert aliandika.

Hivi “kasayole” ni nini jamani….mkiamka naomba mnisaidie!!

A post shared by Rama Dee Master Wa Hizi Mambo (@ramadeeofficial) on

Hata hivyo Rama Dee katika wimbo huo uliotayarishwa na producer Elly Da Bway, alikutana na pongezi na sifa juu ya ufundi wake katika wimbo huku idadi kubwa ya mashabiki katika maoni ikiomba wimbo huo uandaliwa video kwani ni wimbo mzuri.

Comments

comments

You may also like ...