Header

Diamond Platnumz na mrembo Tunda wamtoa maneno Zari The BossLady

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz ameanza kuhusishwa na tetesi za mrembo video Vixen kutoka Tanzania Tunda kuwa mjamzito na hili linaonekana kufanana kabisa na lile la mwaka jana kuhusu Hamisa Mobeto kwakuwa mbali na Hamisa kuwa alishiriki kama Video Queen pia Tunda naye alishiriki katika video ya Salome.

Mara hii uvumi unafanana kwa maana kuwa tetesi za ujauzito alionao Tunda inasemekana kuwa ni wa Diamond Platnumz lakini Diamond kwa kipindi ambacho anahusishwa na uvumi huu, kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha yake yenye ujumbe wenye ishara za kuwa ni kama anaweka neno juu ya hizo tetesi zinazomjumuhisha.

Aliandika “Eti Diamond Madale Kang’ung’aniwa…. Mxiiiew!” na hiki kilichoandikwa kina maana ya kuwa Diamond Platnumz anayohamu ya kuwafahamisha  jambo wote wanaohisi tetesi zinaweza kuwa na ukweli ndani yake.

Hata hivyo kwa Upande wa Zari, hiki cha Diamond na Tunda kimemtoa maneno kwani imeonekana tetesi hizo za Ujauzito wa Tunda kuwa ni wa Diamond Platnumz zimemfikia na aliweka jumbe mbili tofauti katika mtandao wa Snapchat kwa kuandika “Ati madale state Lodge or Madale Guest House? Kuna mtu alikuwa anauliza akipanda bajaji anashukia wapi” ujumbe ambao ulitafsiriwa kuwa ni dongo kwa Tunda.

Lakini hakuishia hapo ambapo alipost picha nyingine akiwa katika hali ya mshangao na kuandika “Mama yangu sio state haouse tena….” hapa anamaanisha nyumba ya Diamond Platnumz iliyoko Madale kama kwa kinachosemekana kina ukweli basi sio State house tena.

Maswali ni mengi ya meibuka juu ya hili lakini kila mmoja anayo hamu ya kujua ukweli wa ni upi na ni kipi kinapelekea haya kuzungumzwa kwa kiasi kikubwa.

Comments

comments

You may also like ...