Header

Joh Makini: Mimi na Fid Q hatuna matatizo kama watu wanavyofikiri

Joh Makini amezikanusha tetesi zilizopo mtaani kwa muda mrefu kuwa yeye na Fid Q haziivi. Ameeleza kuwa hawajaweza kufanya wimbo wa pamoja hadi sasa kwakuwa bado hawajawahi kukutana kwenye mazingira hayo.

Kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times FM, Joh amesema, “Binafsi sijawahi kuwa na matatizo naye [Fid], na wala sijawahi kuona kwamba ana matatizo na mimi so mimi kama msanii, yeye kama msanii anything can happen, anytime. Ni vile tu hatujawahi kukutana kwenye hiyo vibe, hatujawa kwenye hiyo chemistry ya kufanya kazi pamoja, so you never know.”

Fid naye amewahi kuelezea kitu kama hicho hicho kwenye mahojiano ya awali na kudai kuwa yeye na Joh hawana shida yoyote.

Comments

comments

You may also like ...