Header

Vanessa Mdee apata ruksa ya ‘Pumzi ya Mwisho’ kutoka kwa Familia ya Mbaraka Mwinshehe

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Vanessa Mdee ameitembelea familia ya mkongwe wa muziki Marehemu Mbaraka Mwinshehe kupata Baraka na ruhusa ya kutumia kionjo cha wimbo wa ‘Jogoo la Shamba’ kilichosikika katika wimbo wa ‘Pumzi ya Mwisho’ uliowashirikisha Rapa ‘Cassper Nyovest’ kutoka Afrika Kusini na Rapa Joh Makini kutoka Tanzania.

Kolabo hiyo iliyotayarishwa na producer anayepanda kwa kasi S2Kizzy katika studio za Switch Records, imepata Baraka za kutosha kutoka kwa wanafamilia katika makubaliano kuwa watanufaika kwa kupata nusu ya mauzo ya wimbo huo yatakayopatikana katika mapato ya kidigitali.

“Pumzi ya mwisho ni wimbo ninao upenda sana kwenye ulbum yangu ya #MondayMondays. Ni moja kati ya nyimbo zangu bora kwenye album. Sababu kubwa ya Mimi kuchagua beat ya huu mwimbo ni kionjo kimoja kutoka kwenye wimbo wa hayati MBARAKA MWINSHEHE #Legend kabla ya album kutoka nikaona ni vema kuwaona familia ya MBARAKA kwanza ili nipate idhini ya kuendelea na kazi hiyo na kuona watanufaika vipi kama familia kupitika huo wimbo. Nashukuru walinipokea vizuri sana na walitoa idhini yao kwa mikono miwili kabisa. Nusu ya mauzo ya wimbo huu kwenye mitandao ya kidigitali yataenda kwenye familia ya Mzee Mwinshehe siku zote. Nisingeweza kukamilisha kazi hii bila mkono wa @s2kizzy producer, Sauti ya @CassperNvoyest kutoka #SouthAfrica na Mwamba @johmakini asanteni sana. Kuna mengi tuliongea kuhusu mzee ya kusikitisha na kufurahisha pia unaweza kuona video yote ukiwa na #VeeMoneyAppinapatikana kwenye store zote #PlayStorena #AppStore Asanteni sana #MoneyMondays #PumziYaMwisho

Video ya Vanessa akiwa na wanafamilia na mjane wa Mabraka

Pumzi ya mwisho ni wimbo ninao upenda sana kwenye ulbum yangu ya #MondayMondays. Ni moja kati ya nyimbo zangu bora kwenye album. Sababu kubwa ya Mimi kuchagua beat ya huu mwimbo ni kionjo kimoja kutoka kwenye wimbo wa hayati MBARAKA MWINSHEHE #Legend kabla ya album kutoka nikaona ni vema kuwaona familia ya MBARAKA kwanza ili nipate idhini ya kuendelea na kazi hiyo na kuona watanufaika vipi kama familia kupitika huo wimbo. Nashukuru walinipokea vizuri sana na walitoa idhini yao kwa mikono miwili kabisa. Nusu ya mauzo ya wimbo huu kwenye mitandao ya kidigitali yataenda kwenye familia ya Mzee Mwinshehe siku zote. Nisingeweza kukamilisha kazi hii bila mkono wa @s2kizzy producer, Sauti ya @CassperNvoyest kutoka #SouthAfrica na Mwamba @johmakini asanteni sana. Kuna mengi tuliongea kuhusu mzee ya kusikitisha na kufurahisha pia unaweza kuona video yote ukiwa na #VeeMoneyApp inapatikana kwenye store zote #PlayStore na #AppStore Asanteni sana #MoneyMondays #PumziYaMwisho

A post shared by VeeMoney (@vanessamdee) on

Hata hivyo Vanessa Mdee ameendelea kufanya vizuri kwa kuzungumziwa vyema juu ya ubora wa kazi zilizokamilisha idadi ya ngoma 17 katika album ya Money Mondays.

Comments

comments

You may also like ...