Header

Barakah The Prince akerwa na Udhalilishaji wa anayejiita Nabii, Aomba adhabu ya kunyongwa

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Barakah Andrea ‘Barakah The Prince’ amekerwa na vitendo vya mtu aliyejitambulisha kwa jina la Nabii Tito anayesambaza ujumbe na kufanya ibada sambamba na ulevi kwa msisitizo wa matumizi ya pombe na kuoa wanawake zaidi ya mmoja kwa kivuli cha uamini wa Mungu.

Kupitia ukurasa wa Instagram Barakah ameweka kipande kifupi cha video ya Nabii huyo akiendesha ibada kwa mifano ya kuonesha kwa uhalisia matumizi ya pombe na mapenzi kwa mwanamke zaidi ya mmoja ambapo Barakah ameviomba vyombo husika kumchukulia hatua kali za kisheria ili kukomesha hali hiyo anayoendelea kushamiri kwani ila kila dalili za udhalilishaji, kinyume na tamaduni na Desturi za mtanzania.

“Kama ningekuwa na mamlaka katika Nchi hii basi uyu mtu ningeandaa sherehe ya kitaifa ya KUMNYONGA mbele ya mamilion ya watu..Tucheze na vyote na sio kucheza na imani ya watu,na kudhalilisha wanawake ambao ndio mama zetu..enyi vyombo husika hii ipo nje ya maadili ya taifa letu..ningependa uyu bwana apewe adhabu niliyoiomba hapo juu..na ifanyike sherehe kubwa ya kitaifa..” Aaliandika Barakah.

POST YA BARAKAH THE PRINCE.

Hata hivyo Barakah alitafsiri vitendo vya Nabii huyo kuwa ni udhalilisha mkubwa wa akina mama na uvunjifu wa misingi ya kiimani kwa baadhi ya waaminio nje ya Imani na uabudu wa Nabii huyu bila kujali nini malengo ya mtu huyo ambaye uendesha ibada na wake zake.

Comments

comments

You may also like ...