Header

Michael Carrick akubali Ofa ya Mourinho

Kiungo wa Klabu ya  Manchester United Michael Carrick ametangaza kuwa atastaafu mwishoni mwa Msimu huu wa 2018 na amekubali ofa ya Jose Mourinho ya kuwa miongoni mwa Makocha katika benchi la Manchester.

Carrick, 36 ambaye hajacheza Mchezo wowote tangu Mwezi Septemba Mwaka Jana 2017 kufuatia kusumbuliwa na Majeruhi amekubali kujiunga na Benchi la Ufundi la Manchester United pindi Msimu huu ukiisha ofa ambayo Jose Mourinho alimpa tangu mwezi Novemba.

Kiungo huyo ambaye alitangazwa na Mourinho kuwa Nahodha wa kikosi hicho Msimu huu alijiunga na Manchester United Mwaka 2006 akitokea Tottenham Hotspurs akicheza Michezo 314 akifunga jumla ya Magoli 17. Meshinda mataji mbalimbali ikiwemo Ubingwa wa Ligi kuu nchini England mara tano, UEFA Champions league mara moja Mwka 2008 pamoja na Ubingwa wa EUROPA mwaka Jana.

 

 

Comments

comments

You may also like ...