Header

Msemaji wa Nguli wa Soka nchini Brazil Pele akanusha taarifa za Hosptali

Brazilian soccer star Pele displays the FIFA World Cup during its presentation in Rio de Janeiro in February 2010. Pele's World Cup winner's medals from 1958, 1962 and 1970 are up for auction

Nguli wa Soka kutoka Brazil Edson Arantes do Nascimento maarufu kwa jina la Pele amepumzishwa Nyumbani kwake na wala si Hosptali kama ilivyodaiwa kuwa alipelekwa kufuatia kuanguka gafla kwa kile kinachodaiwa ni Uchovu.

Taarifa iliyotoka Ijumaa ilikuwa inaeleza kuwa Pele, 77 alipelekwa Hosptali lakini Msemaji wa Mchezaji huyo amekanusha taarifa hizo zilizozagaa katika Mitandao mingi nchini Brazil

“Habari za Uongo, Pele hakutaka kwenda Hosptali sababu alijua tu atachishwa na kuzungushwa na itazidi kumuongezea Mawazo tu” Alisema Msemaji wake.

Pele ambaye ni Mchezaji pekee kushinda Taji la Kombe la Dunia mara tatu (1958, 1962 na 1970.), amekuwa akisumbuliwa na Matatizo ya Figo kwa Miaka ya hivi karibuni ambayo yamekuwa yakimzuia katika kuhudhulia shughuli mbalimbali ikiwemo kukosa ufunguzi wa Mashindano ya Olimpic Mwaka 2016 yaliyofanyika Rio de Jenairo nchini Brazil.

 

Comments

comments

You may also like ...