Header

“sijajua Ngoma ipi imefanya vizuri kati ya ‘kilio’ na ‘utatulia”:- Lava Lava

Msanii kutoka WCB Lavalava anaefanya vizuri na ngoma zake ikiwemo ‘UTATULIA’ amekiri kuwa mpaka sasa hana jibu kamili ni ngoma ipi imepata mapokezi mazuri kati ya Kilio pamoja na Utatulia ambazo ameachia ndani ya Mwezi mmoja.

Dizzimonline imemtafuta Lava lava ambae alikaa kimya kwa mda mrefu baada ya kutoa ngoma yake ya kwanza ya “BORA TUACHANE” ili kutaka kufahamu Wimbo upi anahisi Mashabiki wake wameupokea kwa nguvu lakini Lava Lava  amesema hana jibu ni upi umefanya poa mkali huyo  amesema ametoa kazi ambazo mashabiki wengi walikuwa wanatamani kuzipata kwa muda mrefu.

“unajua nyimbo zote zimepokelewa vizuri kwasababu tunaona kila nyimbo tukijaribu kurecord clip kidogo watu wanaiomba kwa wingi na ikifika mtaani watu wanasema ngoma kali, kweli Lavalava mwaka huu umeamua kutukomoa umeachia ngoma kali  yani kila nyimbo inakata kiu na zinaburudisha na kwasasa swezi kusema bora ipi kwasababu bado muda ni mfupi tangu niziachie so tusubiri subiri kidogo” amesema Lavalava.

Hata hivyo Lava Lava amesema kuwa ataendelea na Speed hii ya kuachai nyimbo kali kwa muda mfupi hasa kwa Mwaka 2018 hivyo ,Mashabiki wake wakae mkao wa kula na kuendelea kumpa Support katika Mziki wake.

Comments

comments

You may also like ...