Header

“Siwezi kuwa Single”;- Jackline Wolper

Msanii kutoka Bongo Movie ambaye pia ni Mjasiriamali Jackline Massawe Wolper ameibuka na lingine kwa kudai kuwa  licha ya misuko suko yote anayo pitia kwenye mahusiano yake hayawezi kumfanya aishi bila kuwa na mahusiano yaani kuwa single

Staa huyo ambaye ni Moja kati ya mastaa wa tamthiliya ya Kapuni amepiga story na Dizzim Online na kusema hana sababu ya kuwa single wakati ni mtoto wa kike na anavutia na kila siku amekuwa akipokea maombi mbali mbali yakutakwa na Wanaume wenye kila sifa na mionekano tofauti.

‘siwezi kuwa single jamani natongozwa sana sana akili ni kwamba natakiwa kubadilisha aina zile za wanaume wa mara ya kwanza nikisema niwe single nitaongopa maana maombi kila siku na mengi sana  watu wanashusha CV zao  so nikuchuja tu na tayari nishachuja  nimeona  mmoja ndie namchunguza  nipo nae  nipo nae kwasasa  na ni mkaka mkubwa tu  sio tena vijana  wanaotafuta kutoka kupitia mimi ‘ amesema Mrembo huyo

Wolper alishawai kuwa kwenye mahusiano na Harmonize,Brown ingawa mahusiano hayo hayakudumu kwa muda mrefu anadaiwa pia kufunga Ndoa na Msanii Engine licha ya kuhusishwa pia kuwa katika Mahusiano na Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania anayeishi Kenya Sappy.

Comments

comments

You may also like ...