Header

‘Wino Mweusi ni kitabu sio Wimbo” Dogo Janja

Msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Abdulaziz  Chende a.k.a Dogo Janjaro ameitoa maana halisi ya yeye kuandika caption zenye mafunzo na maana tofauti fofauti zikiwa zimegubikwa na mafumbo kuwa ni misemo inayopatikana katika kitabu chake anachokitarajia kutoa hivi karibuni.

Akipiga story na DizzimOnline Rapper huyo kutoka ngarenaro ambaye ni mume wa mrembo kutoka bongo movie Irene Uwoya  amesema kila  analolifanya lina sababu zake kwani hata na hili la kuweka caption zenye ujumbe mkali kwenye instagram yake pia anamaana yake.

 

‘kuna kitu kikubwa kinakuja  kinahusiana na wino mweusi yaani nakuja na kitabu ambacho kinaitwa wino mweusi na kitahusiana na vitu vingi tu sana ikiwemo maisha na asilimi 95 itakuwa inalenga jamii na katika kitabu hiko tumeandika watu wawili mimi na Madee ingawa mpaka hivi sasa sijajua kama tutakiachia bure au tutauza”. alisema Dogojanja

 

Janjaro amewaomba mashabiki zake watowe support kubwa pindi watakapo kiachia kitambu hiko ambacho anaimani kitakuwa na mafunzo mengi sana.

Comments

comments

You may also like ...