Header

Engine autetea ukaribu wake na Wolper

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Engine ameelezea  ukaribu wake na msanii wa Bongo Movie ‘Jackline Wolper’ baada ya tetesi zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa mahusiano yake na Wolper sio ya kimapenzi.

Akizungumza na Dizzim Online Engine amesema kuwa yeye na Jackline Wolper ukaribu wao hauwezi kuvunjika kwa maneno ya watu kwa kuwa kitu kingine kinachowaunganisha ni juhudi zao za kazi.

“ki ukweli ukaribu wangu na Wolper hauwezi kufutika hata siku moja na ndio maana umeniona bado nipo nae mpaka tunatambulisha nyimbo  alafu mimi na Jack tofauti na mambo mengine  tunaingiliana katika kazi tunazo zifanya. Mimi ni producer mimi ni msanii  mimi natunga  mimi ni director, naweza nikamtungia nyimbo, movie nikamshoot nikamueditia nikampa  so utendaji wangu wa kazi na juhudi zangu ndio utakao endelea kunikutanisha na Jack”. Amesema Engine.

Hata hivyo Engine hakuwa na idadi kubwa ya mashabiki na alianza kuzungumziwa zaidi baada ya kuanbza kusambaa kwa tetesi kuwa kuwa yupo kwenye mahusiano na mrembo Jackline Wolper.

Comments

comments

You may also like ...