Header

MC Jessy kusimika mizizi zaidi Churchill Show

Mchekeshaji Mweza wa kipindi maarufu cha uchekeshaji cha nchini Kenya, Churchill Show, MC Jessy amezungumzia mipango yake ya kuendelea au kujiondoa katika muunganiko wa kipindi hicho kutoka na kuwa kwa sasa ni mchekeshaji mkubwa na hali kwake itakuwaje kulingana na wenzake walioonekana kupata majina makubwa na kuamua kujiondoa kisha kutengeneza njia zao za kibishara.

MC Jessy amekuwa akionekana kuwa ni mhusika anayefuata katika viwango na ubora wa uchekeshaji na kiungozi na akichokisema kuhusu yeye kudumu katika kipindi hicho cha uchekeshaji, amesema kuwa anaamini kipindi hicho bado ni kidogo hivyo mpango wa kukiendeleza na kukikuza uko pale pale na upo mpango wa kuanzisha kipindi kingine ili kujikuza zaidi.

“Pekee yako you can only go so far. But together you can go far. Our partnership is way beyond money. We are going to launch new shows this year, cause the Churchill Show is too small,” Amesema Jessy.

Hata hivyo kati ya mastaa wa uchekeshaji kutoka Kenya waliopita katika kipindi cha Churchill(Churchill Show) kisha kuanza kufanya kazi zao katika misingi ya kujitegemea ni pamoja na Eric Omondi, Chipukeezy, Teacher Wanjiku na wengine.

 

Chanzo: Ghafla

Comments

comments

You may also like ...