Header

Mdernmark Caroline Wozniacki aweka rekodi na kushinda Australian Open 2018

Mwanadada Caroline Wozniacki kutoka Dernmark amefanikiwa kushinda Taji la Australian Open kwa Upande wa Wanawake baada ya kumfunga Simona Halep kutoka Romania katika Mchezo wa Fainali uliopigwa Melbourne Park.

Wozniacki ameshinda kwa Seti 7-6 (7-2) 3-6 6-4 ikiwa ni Mara yake ya kwanza kushinda Ubingwa wa Grand Slam na kumfanya apande katika Viwango vya Ubora kwa upande wa Wanawake Mpaka nafasi ya kwanza akimpiku  Mpinzani wake Simona Halep aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo.

Kwa upande wa Wanaume Mchezo wa fainali utapigwa Kesho Januari 28 kati ya Cilic dhidi ya Federer, Mchezo unaosubiriwa kwa hamu ili kujua nambari moja mpya kwa upande wa Wanaume

 

 

Comments

comments

You may also like ...