Header

Rick Ross na Diamond Platnumz ni maswali bila majibu

Ni kipindi ambacho bado hatujapata jibu la kwanini Rap kutoka Marekani Rick Ross ameondoa picha baadhi za Staa wa muziki kutoka Tanzania , Diamond Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo baadhi ya watu alihisi kama kuna kutoelewana kati yao na sasa kitu kingine kimejitokeza ambacho ni Rick Ross kupost picha ya chupa za Mvinyo wa Belaire na kuwatag mastaa kibao wanahusika na kinywaji hicho.

Kati ya mastaa waliotagiwa ni pamoja na Kundi la muziki wa rap kutoka Marekani la Migos, Diddy, Meek Mill, Dj Khaled pamoja na Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambapo muda mfupi baadae Rick Ross aliondoa Post hiyo kwenye ukurasa wake.

Diamond Platnumz na Rick Ross walishirikiana kwenye kazi ya WAKA WAKA ambayo mpaka sasa imefanya vizuri hasa kwenye mtandao wa YouTube kwa kupata kutazamwa kwa zaidi ya mara Milioni 5 ndani ya muda wa mwezi mmoja na hili la kuweka na kuondoa picha linabaki likiwachanganya mashabiki wa Diamond Platnumz wasijue ni nini kinaendelea kati ya Rick Ross, Balaire na Diamond Platnumz katika kipindi ambacho unasubiriwa ujio wa Album ya Diamond Platnumz ya A BOY FROM TANDALE itakayotoka rasmi .tarehe 23 Februari mwaka huu.

Hata hivyo Diamond Platnumz bado anaendelea kuoneakan katika page rasmi ya Belaire kwani ile picha aliyopostiwa siku tano zilizopita akiwa ameshikilia chupa mbili za kinywaji hicho bado ipo kwenye ukurasa huo.

Comments

comments

You may also like ...