Header

Mr. T ajitambulisha kama msanii kwenye kolabo ya Gaga Blue na Barakah The Prince

Msanii kutoka Burundi, Gaga Blue baada ya kuachia video ya wimbo wake mwaka jana kwa jina la ‘Nakupenda’ akiwa nchini Tanzania, ameachia video ya nyingine wimbo wake mpya kwa jina ‘Mama la Mama’ na mara hii kitu cha tofauti mbali na kuwa amemshirikisha Barakah The Prince, Watayarishaji wa ngoma hiyo ambao ni ni Davy Makodi na Mr T Touch , Mr. T Touch ameshirikishwa na amesikika katika mdundo akipanga kwa uzuri michano mithiri ya rap mwenye ujuzi na uzoefu.

Mr. T katika kipindi ambacho amezungumziwa zaidi kwa kufanya hit song nyingi, michano aliyoiachia katika wimbo huu mpya wa Gaga Blue inaweza kukubalika kuwa Mr. T ni zaidi ya mtayarishaji kwa maana ya kuwa pia unaweza kumuita mchanaji(Rapa).

Video ya wimbo huo imepambwa kwa warembo na rangi zilizopendezesha kioo cha mtazamaji kwa uongozaji wa Director Destro chini ya Wanene Filmz.

Itazame video hii mpya ya Gaga Blue

Comments

comments

You may also like ...