Header

Bekaflavour atoa sababu za kutofika kwenye utambulisho wa Mbosso

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Bekari Abdul a.k.a Bekaflavour  ametoa sababu ya kutohudhuria kwenye utambulisho wa aliyewahi kuwa msanii mwenzie kwenye Band moja ya “Yamoto Band” Mbosso

Akizungumza na Dizzim Online msanii huyo anayetamba na Ngoma ya Sikinai amesema kuwa hakuna sababu kubwa ni kucheleweshwa kwa kadi ya mualiko hivyo alishindwa kujiandaa na kufika kwa wakati kwenye sherehe iliyofanyika Hayatt Regency Posta

“Taarifa niliipata ila cardy nilicheleweshewa kuipata na ikawa siku ambayo ndio anatambulishwa mimi nipo location nashoot nyimbo yangu nafika nyumbani usiku ndo nakutana na card yani ile ile siku kwa usiku wake ule ule ndo naletewa card so mimi sikuwahi kwenda lakini meneja wangu aliniwakilisha.” amesema Bekaflavour.

Aidha msanii huyo amewaomba watanzania wampe support kubwa mboso kwenye ujio wake huo kwani anaamini ni msanii atakae ufikisha mbali muziki wa Bongo fleva.

Comments

comments

You may also like ...