Header

Idris Sultan na jasho lake katika Safari ya Hollywood

Idris Sultan ni Staa wa burudani kutoka Tanzania, ambaye kwa sasa ameshajitokeza katika nyanja kadhaa na zaidi wengi wakimuona na kutarajia mengi katika upande wa tasnia ya maigizo huku yeye akionekana kutengeneza njia za kuishi tasnia hiyo katika viwango vya kimataifa na wiki hii bado anategemea kutakiwa mema na maisha marefu kwani ni wiki yenye tarehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake(Januari 28 1993).

Idris anaaminika kuwa ni mmoja kati ya vijana wenye ushawishi mkubwaTanzania na moja ya mipango na ndoto zake ni kuwa muigizaji Mtanzania atakayejizolea umaarufu na mashabiki wengi zaidi Duniani kwa kufanya kazi zenye ushirikiano mkubwa na waandaaji pamoja na waigizaji wa kimataifa zaidi kutoka Hollywood kitu kitakacho ongeza heshima kwa taifa la Tanzania, tasnia ya filamu Tanzania(Bongo Movie) na kuongezeka thamani yake na Brand yake kwa ujumla.

Kwa Tanzania wapo ambao wameshaanza kuona na kuridhika kutokana na kasi ya safari hiyo ya Idris kwani tayari ameashanza kuonekana na kuonesha uwezo wake kupitia kazi nzuri na kubwa za maigizo ambazo zinatajwa kufanya vizuri na katika orodha ya haraka ya kazi alizoshiriki ni pamoja na Filamu ya ‘Kiumeni’na tamthilia ya ‘Kapuni’.

Comments

comments

You may also like ...