Header

Mo Music azipiga kikumbo kiki za muziki kwenye kazi zake

Msanii wa muziki wa kizazi wa kipya kutoka Tanzania, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amepinga mawazo ya yeyote atakayejaribu kuhusisha muziki wake na suala la kiki kwa nia ya kuachia kazi ili apate kuzungumziwa zaidi kama inavyotokea kwa baadhi ya wasanii.

Akipiga Stori na Dizzim Online, Mo amesema kuwa wapo wanaoamini katika kiki ili muziki wao ufike na hilo sio tatizo kama wanafanikisha lakini kwake sio jambo lenye nafasi katika muziki wake kwani amaanini katika muziki mzuri na bidii linapokuja suala la kufanya kazi kama msanii.

“Unajua nitashangaa sana kama nitakutana na malalamiko au minong’ono ya kuwa muziki wangu unaenda sambamba na Kiki, sio kweli na sio mambo yangu kabisa. Mimi nikizungumziwa ujue ni kazi tu na sio vinginevyo kama inavyofanyika kwa baadhi ya wasanii hasa hasa hapa Kwetu(Tanzania). Napenda kufanya kazi na sio kufanya kiki ili niskike, ikitokea nimezungumziwa nje ya kazi basi kuna mtu kasababisha iwe hivyo” Amesema Mo Music.

Comments

comments

You may also like ...