Header

Tunda atolea ufafanuzi kwa kinachoendelea mitandaoni

Model na Video Vixen kutoka Tanzania Tunda Sebastian a.k.a Tunda the Boss babe ametolea ufafanuzi juu ya kinachoendelea kati yake na msanii wa bongo Movie Aunty Ezekiel baada ya kutupiana maneno makali kwenye mtandao wa Instagram kufuatia madai ya Aunty kumdai Tunda pesa ya pombe aliyochukuwa dukani kwake.

Akipiga story na DizzimOnline mrembo huyo anayeuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo ambaye pia anahusishwa kutoka kimapenzi na msanii Diamond Platnumz amesema pesa alilipa isipokuwa Aunty anatafuta promo ya duka lake.

“Huyo Aunty nilichukuwa pombe dukani kwake hakunipa yeye alinipa Mose  ilikuwa muda umeisha  na duka lilikuwa limefungwa  kwenye saa8 usiku tena moja  nikampa na hela dizaini kama Mose hizo hela hajazifikisha kwa mke wake sasa Aunty ananiandikia vile  Instagram  sijaelewa anamaanisha nini  na bwana wake nampigia simu hapokei kwahiyo hapo bwana wake ndio kaipiga hiyo pesa alafu kwanini asitafute namba yangu akanipiga kwasababu anataka watu wamuongelee  na chuki zake za chini chini.” amesema Tunda.

Tunda  ambaye kwasasa amekuwa akizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii baada ya kuvuja kwa video yake ya kimahaba na mwanaume maarufu kwa jina la Kinje ambaye ni mume wa mtu .

Comments

comments

You may also like ...