Header

Philadelphia Eagles yaweka Historia Super Bowl, yapeleka ushindi kwa Meek Mill

Timu ya Philadephia Eagles imefanikiwa kushinda Taji la Super Bowl 2018 kwa mara ya kwanza katika historia baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya New England Patriots kwa jumla ya alama 41-33 katika Dimba la Bank Stadium huko nchini Marekani.

ukiachana na historia hiyo iliyowekwa na Philadephia kitu kingine kikubwa kilichovuta hisia za Mashabiki wa Mchezo huo ni kitendo cha timu hiyo kuvaa Jezi ambazo nyuma ziliandikwa maandishi yaliyosomeka hivi Free Meekmill yaani “Meek Mill aachiwe huru”.

Rapa Meek Mill ambaye anatumikia kifungo cha Miaka Miwili ni Shabiki Mkubwa wa timu hiyo ambayo ni timu yake ya Nyumbani, Licha ya kutokuwepo Uwanjani lakini Wachezaji hao pamoja na Mashabiki walionyesha kupinga kitendo cha Meek Mill kufungwa huku wakiendelea kuungwa Mkono Harakati za kumuachia huru Meek Mill.

 

 

 

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...