Header

Bongo Movie Tujifunze Mengi kutoka kwa Waigizaji wa China:- Natasha

Mkongwe wa Sanaa nchini Tanzania Natasha ambaye ni Maarufu kwa jina la Mama Monalisa ameleza kuwa ni wakati sasa wa Waigizaji wa Tanzania kujifunza mengi kupitia Tamthiliya kutoka China kwani Utamaduni wao na wetu hautofautiani Sana katika Maisha ya Kila siku na pia wamepiga hatua kubwa sana katika Sanaa.

Natasha amesema hayo wakati wa Hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya uuzaji na usamabaji wa Ving’amuzi ya Startimes ambayo ilikua na Lengo la kuwakutanisha Wasanii wa Bongo Movie pamoja na Muigizaji aliyejizolea umaarufu nchini kupitia Tamthiliya ya Mau Dou Dou na Wakwe zake Hai Qing ‘Mau Dou Dou’.

“Nilikuwa nafuatilia Sana Tamthiliya ya Mau Dou Dou na wakwe zake, nimeona kabisa Utamaduni wao na wetu hauna Utofauti Sana na ukiangalia wenzetu wamefanikiwa Sana katika Sanaa nadhani ni Muda sasa wa sisi kujifunza Mengi sana kupitia Mau Dou Dou kuja hapa lakini pia tujifunze mengi kupitia Tamthiliya za China”. Alisema Natasha.

Kampuni ya Star Media (T) Ltd kupitia chapa yake ya StarTimes imefanya hafla hiyo yenye Lengo la kumkutanisha muigizaji maarufu wa China Hai Qing maarufu kama Mau Dou Dou na wasanii wa kitanzania pamoja na mashabiki wake, Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (NICC) na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali maarufu akiwemo Natasha, Yvone na Davina pamoja na Dullvani.

Comments

comments

You may also like ...