Header

Gari la Diamond Platnumz lapewa muonekano mpya na wa kisasa

Staa wa Bongo Fleva kutoka Nchini Tanzania, Naseeb Abdul Juma ‘Diamond Platnumz’ siku sio nyingi anategemewa kuanza kuonekana akisukuma mkoko wake uliopewa muonekano mpya na kampuni ya kupimp magari jijini Dar es Salaam, Tanzania #TttraoutGrades.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa kampuni hiyo umekuwa ukipost juu ya ukaribu wa Staa huyo hata kuonesha kuwa kuna dalili za kufanya nao kazi ambapo Diamond Platnumz akiwa na Meneja wake Babu Tale alionekana katika ofisi za kampuni hiyo, kipindi ambacho inaaminika kuwa Diamond alitembelea ofisi hiyo kwa lengo la kuwapa jukumu la kunogesha muonekano wa gari lake aina ya BMW X6.

Muonekano wa Awali wa Gari la Dizmond Platnumz

Mapema leo kampuni hiyo kupitia ukurasa wake huo ilipost muonekano mpya wa gari hilo lililokuwa katika muonekano wa rangi nyeusi likiwa katika muonekano mpya wa rangi ya blue yenye kung’aa na kuandika ujumbe wenye ishara ya kuwa sasa Diamond Platnumz anaweza kuendelea kutumia gari lake liliopewa muonekano maridadi kabisa.

Huu ndo muonekano mpya wa Gari la @diamondplatnumz

A post shared by Dizzim Online (@dizzimonline) on

Comments

comments

You may also like ...