Header

Hiki ndo kinachongojewa katika Simulizi ya tamthilia ya Sarafu

Wakati mashabiki wakiwa wanaingoja kwa hamu sehemu ya tisa ya tamthilia ya Sarafu, hebu tuangalie yaliojiri wiki zilizopita! Chuki kati ya Engineer Sanga na Engineer Samwel inazidi kupamba moto huku kila mmoja akifanya juu chini kumteketeza mwenzake, huku wake zao nao wakiwatuhumu  kuwa ni wasaliti wa ndoa kwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanawake wengine nje ya ndoa.

Jacky na Janeth ni mabinti wa Eng. Sanga. Kila mmoja ana matatizo kutokana na changamoto zilizotoka katika familia yao. Jacky (Elizabeth Michael Lulu) anahisi wazazi wake hawampendi kama wanavyompenda Janeth (Irene Uwoya) hivyo Jacky anaishi maisha yake kuwakomoa wazazi wake kwa kuwa na mahusiano na adui mkubwa wa baba yake.

Upande mwingine, Tuna kijana Chuma (Idris Sultan) ambae yupo gerezani na ni mpenzi wa muda mrefu wa Jacky (Lulu). Jacky anajaribu juu chini kushikilia penzi lao lakini huku uraiani Jacky anaishi Maisha ambayo Chuma hajui chochote.

Je mahusiano yao yataishia wapi? Kutana na kijana mwingine anayeitwa Damian (Hemmed PHD) Damian mtoto wa Eng. Samwel mpenzi wa Janeth (Irene Uwoya) lakini mapenzi yao yemeingia doa baada ya Damian kugundua Mpenzi wake anatoka na Baba yake Mzazi kitu kilichopelekea uhasama wa kimapenzi kati yake na baba yake Mzazi bila ya kufahamu kuwa Janeth ametumwa na adui yao (Eng.

Sanga Baba wa Janeth) kumlaghai huku wakiwa na njama zao binafsi! Usikose muendelezo wa Tamthilia hii ya Sarafu inayoruka kila Jumatano na Alhamisi kupitia chaneli ya DStv Maisha Magic Bongo ya kifurushi Bomba kwa sh.19,000 tu

Comments

comments

You may also like ...