Header

Lionel Messi amkaribisha mtoto wake wa Tatu ‘Ciro’ katika Familia

Staa wa Klabu ya Soka ya Barcelona Lionel Messi ameonekana kuweka wazi jina la mtoto wake wa Tatu ambaye anatarajia kuzaliwa hivi karibuni na Mkewe, Mwanadada Antonella Rocuzzo.

Wawili hao wanatarajia Mtoto wao wa Tatu mwenye Jinsia ya Kiume kati ya Mwezi huu wa Februari mwishoni au Machi mwanzoni ambaye Messi ameliweka wazi jina la Mtotot huyo kuwa ataitwa Ciro.

Familia de 5❤️❤️❤️❤️❤️ #blessed👦🏻👦🏻👦🏻

A post shared by AntoRoccuzzo88 (@antoroccuzzo88) on

Messi kupitia Mtandao wa kijamii wa Instagram ameweka video sehemu ya ‘Insta story’ inayoonyesha sehemu ya Tumbo la Mkewe huku akiambatanisha na ujumbe kwenye viedo hiyo uliosomeka ‘Baby Ciro’ ambao unadhihirisha wazi kuwa mtoto huyo atakuwa akiitwa jina hilo.

Mpaka sasa Messi na Mkewe wamebarikiwa kupata watoto wawili ambao ni Thiago mwenye Miaka 5 pamoja na Mateo mwenye Miaka Miwili.

Comments

comments

You may also like ...