Header

Diamond Platnumz ashiriki kuandika simulizi ya video katika wimbo wa Mbosso ‘Watakubali’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz ameendelea kukitumia kipaji chake cha sanaa kama muongozaji wa video za nyimbo katika wimbo mpya wa msanii mpya wa WCB Wasafi Mbosso ‘WATAKUBALI’.

Akielezea alichokifanya katika video ya wimbo huo wa Mbosso, Diamond Platnumz amesema kuwa yeye anapenda sana kufanya kazi katika ufanisi na ubunifu kwa lengo la kupata kitu kizuri na katika wimbo wa Watakubali amehusika kuandika mtiririko wa simulizi ya video ya wimbo huo.

“Katika video ya Watakubali nilikuwa ni kama Assistant Director, nilikuwa pia kama Co-Writter wa Stori na pia nilikuwa kama Scene writter. AsMESEMA Diamond Platnumz.

“Unajua Idea ya video zinatokana na nyimbo ya mtu anavyoimba, inatengeneza urahisi wa concept ya video na professionally mimi napenda mambo ya kushoot shoot  kwasababu napenda video nzuri  lakini kabla ya kufanya chochote napenda nisikilize wazo la msanii ameimba na wazo gani…” Ameongeza.

Hata hivyo Video ya wimbo huo wa Mbosso imeongozwa na Director kutoka nchini Afrika Kusini, ‘Nik’ na Diamond Platnumz alishiriki tu katika usaidizi wa kutoa kitu kizuri na video imeshootiwa nchini Tanzania jijini Dar es salaam.

Comments

comments

You may also like ...