Header

Diamond Platnumz atembea peku Mahakamani ndani ya muonekano wa ‘Salome’

Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz mapema leo alienda Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kusikiliza shauri lao la matunzo ya mtoto wake na Hamisa Mobetto ‘Prince Abdul’ ambapo katika muonekano wa mavazi aliyovaa yalizirudisha hisia za wengi katika kumbukumbu ya video ya wimbo wake wa ‘Salome’ aliomshirikisha Rayvanny.

Diamond Platnumz kitu pakee kilichokosa katika muonekano huo wa mavazi ni bakora ambayo kama ingekuwepo basi angekamilisha muonekano wake huo ambao baadhi waliufananisha kwa asilimia kubwa na ule wa video ya Salome ambapo baadae hali isiyotegemewa ilikikuta kiatu chake kupata hitilafu na kusababisha waliowengi kulitolea macho tukio hilo mahakamani pale.

Moja ya picha iliyovunja vunja mitandao ya lkijamii zaidi mtandao wa Instagram ni picha ambayo ilimuonesha akiwa ni mwenye kuketi akiwa peku bila viatu picha iliyodhani kuwa pengine Diamond alikuwa chini ya ulinzi.

Hata hivyo muda baada ya hayo yote kutokea, ulifika Muda wa Diamond Platnumz kuondoka ambapo alizongwa na vifaa vya waandishi wa habari wakitaka kusikia neno kutoka kwake juu ya shauri na makubaliano kati yake na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto ambapo Diamond amesema kuwa kila kitu kiko sawa na wamefikia muafaka lakini endapo mahakama itamhitaji kwa lolote atatoa ushirikiano.

Comments

comments

You may also like ...