Header

Kylie Jenner Avunja Rekodi ya Beyonce Mtandaoni

Warembo wa wawili wenye idadi kubwa ya mashabiki hasa mtandaoni, Kylie Jenner na mama ‘Blue Ivy Carter’ Beyonce wamekutana katika rekodi ya mtandaoni ambayo anayeonekana kufanya vizuri kwa sasa kwa mujibu wa rekodi ya awali ni Kylie Jenner.

Rekodi mpya ya picha kupata LIKES nyingi zaidi katika mtandao wa Instagram imewekwa na KYLIE JENNER kupitia picha yake ya kwanza aliyopost siku ya Jana ‘Jumatano’ ya kumuonesha mtoto wake (Stormi) ambaye amezaa na rapa Travis Scott.

 


Kylie Jenner ameandika rekodi kwa picha hiyo kwa LIKES milioni 14+ kwenye instagram na kwa hilo la likes anavunja rekodi ya Queen B mpenzi wa rapa JAY-Z ‘BEYONCE’ ya likes alizopata kwenye post ya kutegemea watoto mapacha ambayo kufikia hivi sasa imefikia LIKES Milioni 11+ kupitia picha yake ya kwanza iliyopostiwa February 1, 2017.

Comments

comments

You may also like ...