Header

Maana ya Tattoo ya Simba aliyochora Wizkid na Mastaa wengine

Staa wa muziki kutoka Nchini Nigeria, Wizkid Ayo ni mmoja ya msataa kutoka Afrika wenye Tattoo ya Simba wa Kiume kwenye mkono wake wa kushoto na hapa tunakupa maana Tattoo hiyo.

Simba ni moja ya wanyama maarufu zaidi kwa watu na baadhi ya watu uchukua hatua za kuchora tattoo ya SIMBA kwenye miili yao, na utamaduni huu wa uchoraji tatoo hasa kuchora kichwa cha Simba wa kiume ni wa muda mrefu na inawezekana ukawa haujui maana halisi ya mtu kuchora tattoo ya kichwa cha Simba au Simba wa kiume.

Simba au tattoo ya Simba ni ishara ya mtu kujiamini, kuwa na uwezo wa kumiliki imaya yake mwenyewe na ishara kubwa ni kuwa na uwezo wa kuwa na nafasi kubwa katika jamii aliyopo yenye kuweza kufuata nyayo zako na sheria zake pia.

Ishara ya kawaida ambayo inatambulika na maana ya Simba ni Ufalme na kujiamini.

Maana nyingine ya tattoo ya Simba, inaashiria mambo ambayo ni pamoja na ujasiri, ulinzi wa salama, utukufu, ushindi na umiliki wa kijadi(Masculinity).

Chukua hii ukamsimulie mwezako ili usijekudanganywa kuhusu Tattoo ya Simba.

Mtag Staa wako ambaye ungetamani Achore Tattoo ya Simba kulingana na mana yake.

Comments

comments

You may also like ...