Header

“Mtaiona Sura yangu halisi Simba ikishinda Ubingwa”;- Haji Manara

Afisa Habari wa Klabu ya Soka ya Simba Haji Sande Manara ameweka bayana kuwa kwa sasa ameamua kutulia na kukaa kimya bila kuwa na Mchecheto wowote licha ya Simba kuendelea kufanya vizuri Uwanjani na amedai kuwa watu wasubiri pindi Klabu hiyo ikifanikiwa kutwaa Ubingwa ndipo watakapomuona Manara waliyemzoea.

Manara amesema hayo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Makao makuu ya Klabu hiyo Maeneo ya Msimbazi jijini Dar es salaam, Msemaji huyo amesema anajua kuwa Watu wamekuwa wakijiuliza kwanini kapunguza ‘Mbwembwe’.

“Majigambo na kelele nimehamishia kwenye Dakika 90 za Uwanjani, Bado hatujawa Mabingwa kwa sasa. Tukishinda Ubingwa ndipo mtaiona Sura halisi ya Manara na upande wake wa pili mtauona pindi Manara akishinda Ubingwa”. Alisema Manara

Mpaka sasa Klabu ya Simba inaongoza Ligi ikiwa na alama 41 baada ya kuibuka na Ushindi dhidi ya Azam hapo jana huku ikiendelea kuwa Timu pekee ambayo haijapoteza Mchezo wowote ule katika Mochezo 17 iliyocheza huku ikishinda Mechi 12 na kutoka sare Mechi Tano.

Comments

comments

You may also like ...