Header

Ray C aomba aliyeanzisha Social Media alaaniwe, Chanzo ni wanaomsema vibaya Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amethibitishwa kukerwa na maneno yanayosemwa na baadhi ya watu yenye kumpiga vita na kutaka kurudisha nyuma kimaendeleo Diamond Platnumz.

Kupitia picha ya utoto ya Diamond Platnumz, Ray C kwenye ukurasa wake wa Instagram ameshusha lawama zake kwa wanaomsema vibaya kila leo Diamond bila kujali kuwa amekuwa ni mtu mwenye tija na aliyeleta changamoto kubwa za mafanikio katika maendeleo ya muziki wa Tanzania.

“Mi naumiaga sana nikiona huyu mtoto anasemwa semwa kila siku!Amefanya mapinduzi makubwa sana huyu mtoto!kama una macho unaona!Muziki wa Tanzania umefika mbali sana sababu ya watu kama hawa!Nigeria wanafika mbali sana kwa sababu wanasapotiana lakini Bongo sijui kwanini tunapenda kuzodoana!Kushushana!Kuchukiana!Dah!!Yani huyu alieanzisha hizi social media Mungu amlaani!!” Ameandika Ray C.

Hata hivyo hilo la Ray C linaweza kuungana na Maneno ya Meneja wa Diamond Platnumz ‘Sallam Sk’ kuwa wapo wenye nia ya kumuangusha Diamond Platnumz kwa maslahi yao Binafsi jambo ambalo linawakera sana kiasi cha kuhamua kuweka hisia zao katika mitandao ya kijamii.

Comments

comments

You may also like ...