Header

King Fanatic adondosha ya kwanza na Staa wa Dancehall ‘Lord Fenda’

Msanii wa muziki kutoka  DR.Congo mwenye makazi yake yake nchini Uholanzi King Fanatic ameachia kazi yake ya kwanza kwa mwaka 2018 kwa jina ‘Tricky Situation’ akiwa ameshirikiana na Mwimbaji wa miondoko ya Dancehall Lord Fenda.

Kazi hiyo mpya iliyotayarishwa chini ya producer Ray Blaze, video yake imeandaliwa nchini Uholanzi chini ya uongozwaji wa wa kampuni ya Video iliyoko nchini humo ya Trapiex Films.

Katika Mazungumzo na chumba cha habari cha Dizzim Online, King Fanatic amesisitiza kuwa mpango wake wa kutembelea Tanzania kujifunza mengi yanayohusu muziki bado uko pale pale na kikubwa atakachokifanya ni kutembelea baadhi ya maeneo ya vivutio vinavypatikana katika taifa la Tanzania.

“Still is my plan to pay a visit huko, unajua kwa East Africa bado we need to learn a lot about music business especially when it comes to a point of making money. Bado mpango wangu uko tu na nasubiri mambo yangu ya kazi kwasababu tumeajiriwa huku hivyo lazima tuache kila kitu kiko sawa kwanza then tufikirie kufanya mambo mengine” Amesem King fanatic.

Comments

comments

You may also like ...