Header

Rash Don atoa sababu za kutosikika katika kazi za wasanii wakubwa na Wenye Majina kwa sasa.

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania, anayefanya kazi chini ya Studio za Surprise Music ‘Rash The Don’, amesisitiza kuwa ataweka nguvu kubwa katika kufanya kazi na wasanii wachanga wenye kila dalili ya kufika mbali kimuziki na wenye nia ya kutegemea bidii na vipaji vyao katika kazi zao.

Akipiga stori na Dizzim Online Rash ameyasema hayo alipokuwa akitoa sababu za kwanini hasikiki sana katika kufanya kazi na wasanii wa muda mrefu katika muziki na wenye majina na muda mrefu ambapo pia kukanusha uvumi kuwa wasanii wa wenye majina makubwa wanamtenga sana katika kufanya nao kazi.

“Kwanza kuhusu wasanii wakubwa hasa ambao nilishafanya nao kazi kunitenga sio kweli, sema mtu anaweza akasema hivyo kwasababu ya misingi yangu ya sasa. Mimi kwa sasa kama mtu anafatilia atagundua nafanya kazi na wasanii ambao ni wachanga na wanaonekana kuwa na kipaji kikubwa na nawaona mbali. Point yangu ni wasanii wachanga wafaidi kipaji changu” Amesema Rash Don.

Hata hivyo Rashi ametoa orodha yake fupi ya wasanii ambao kwake wana kile anachokimaanisha aliwataja rapa wa kike Rosa Ree, Dogo Janja, na mwimbaji Mbosso anayefanya vizuri kupitia wimbo wake mpya wa WATAKUBALI.

Comments

comments

You may also like ...