Header

“Yanga hatuna Mpango wa kuwashangilia Simba”;- Mkemi

Baada ya kauli ya Afisa Habari wa Klabu ya Soka ya Simba, Haji Manara kuwaomba Mashabiki wa Simba watakaojitokeza kutazama Mchezo wa Yanga dhidi ya St Louis wasiwazomee Yanga katika Mchezo huo wa kimataifa, Klabu ya Yanga yaibuka na kueleza jinsi walivyoipokea Kauli hiyo.

Yanga kupitia kwa Mjumbe wao wa Kamati kuu Salum Mkemi, amemjibu Manara na kusema kuwa lolote lile linaweza kutokea kwenye Mpira wa miguu huku akisistiza kuwa Wao kama yanga hawana mpango wa kuishangilia Simba hata kidogo.

 

Yanga itashuka Uwanjani siku ya Kesho kucheza na St Louis kutoka visiwa vya Sheli Sheli katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ukiwa ni Mchezo wao wa kwanza katika Michuano ya Klabu bingwa Afrika.

 

Comments

comments

You may also like ...