Header

Davido ajipanga kufungua mlango wa nyimbo

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a Davido baada ya kufunga mwaka na wimbo wake wa ‘Like Dat’ ajiweka tayari kuachia wimbo wake mpya utakao fungua mlango wa ngoma zake kwa mwaka 2018.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa twitter na Instagram, Davido amethibitisha kuwa siku ya Jumatatu, wiki ijayo ya tarehe 12 mwezi huu wa Februari anaachia rasmi wambo wake wa kwanza.

“First official single of 2018 drops Monday!! Too Excired” Davido aliandika katika mtandao wa Twitter kisha akamalizia na kitambulishi cha alama ya reli chenye neno #FMF.

🔥⏱🌺

A post shared by Davido Adeleke (@davidoofficial) on

Hata hivyo Davido kwa mwaka 2017 nchini Nigeria alitajwa kufanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa kupata utazamwaji wa mara milioni 100+  kwa video zake 5 pekee za muziki kwa mwaka mzima.

Comments

comments

You may also like ...