Header

Davista aamini njia aliyotengenezewa na Mr Blue kuwa itampeleka mbali

Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Davista ameachia kazi ya pekee yake baada ya ‘Siumii’ aliyomshirikisha Mr Blue , kazi ambayo wiki kabla ilitoka audio kisha rasmi akaachia video chini ya uongozaji wa Director Nisher.

Akipiga stori na Dizzim Online juu ya wimbo wake huo mpya unaokwenda kwa jina ‘Nimekubali’, Davista amesema kuwa kazi hiyo anamini itapokelewa vizuri kwakuwa anaamini Mr. Blue ameshamtegenezea mazingira mazuri ya kuaminika kama msanii mwenye kila sababu ya kupata support kutoka kwa mashabiki.

“Hii kazi naiamni sana kwasababu ni kazi nzuri na kingine ambacho kinanipa imani zaidi na ni kazi yangu niliyoachia mwaka jana niliyomshirikisha Mr. Blue na ujue Blue sio rahisi kumshirikia ujue. Kwanza maani ameniweka katika nafasi nzuri na kutokana na hilo basi naamini mashabiki wataniamini zaidi na watanipa support yao” Amesema Davista.

Comments

comments

You may also like ...