Header

Mwimbaji Ebony Reigns Afariki kwa Ajali

Msanii wa muziki wa dancehall kutoka Ghana Priscilla Opoku-Kwarteng  Ebony Reigns amefariki katika ajali iliyohusisha gari ambalo alikuwa akiendesha na basi la VIP kwenye barabara ya Sunyani kwenda Kumasi, Ghana.

Mwimbaji huyo ambaye angetimiza umri wa miaka 21 wiki ijayo, alikuwa na rafiki yake wa karibu, Franky Kuri, akisindikizwa na ulizi wa kijeshi ambapo katika ajali hiyo hakuna aliyepona.

Ebony alikuwa anafanya kazi chini ya mkataba wa lebo ya muziki ya Rufftown & Midas Touch Inc na tayari alishatoa albamu yake ya kwanza ‘Bonyfied’ iliyopata mapokeo mazuri.

“May her soul and that of the other occupants rest in peace.”

Comments

comments

You may also like ...