Header

Navy Kenzo wamuacha ‘Gold’ Tanzania kwa safari ya kikazi nchini Afrika Kusini

Kundi la muziki kutoka Tanzania linaloundwa na wapenzi, Aika na Nahreel ‘Navy kenzo’ wameandaa na kukamilisha baadhi ya kazi za kundi zilizoko katika mpango wa kutoka rasmi kati kati ya mwaka wa 2018.

Akipiga stori na Dizzim Online, mwakilishi wa kundi hilo ambaye pia ni mtayarisha mkuu wa muziki ‘Nahreel’, amesema kuwa tayari wameshashoot video nchini Afrika Kusini. Nahreel alipoulizwa kama walisafiri na mtoto wao wa kiume ‘Gold’ alisema kuwa safari hiyo ilikuwa ni ya kikazi zaidi hivyo hawakuona sabsbu ya kusafiri na mtoto wao.

Gold

“Dah! hapana…hatukusafiri na mtoto, mtoto ilibidi tumuache kwasababu huko tulienda kikazi na tulihitaji concetration kubwa ya kazi. Gold tuliamuacha kwa mtu wetu wa karibu ambaye alikuwa na jukumu la kumjali na kuhakikisha yuko salama. Naamini alitumiss sana” Alisema Nahreel.

Hata hivyo Nahreel ameongeza kuwa, kuanzia mwezi wa nne mwaka huu(2018) zitatoka kazi kibao kutoka kwake kama Producer, kutoka kwao kama kundi ‘Navy Kenzo‘ na zipo Projects nyingi za wasanii wa ndani na nje ya Tanzania ambazo zimeandaliwa katika viwango vya kimataifa.

Comments

comments

You may also like ...