Header

AY na Mpenzi wake ‘Remmy’ hawakufunga ndoa kama ilivyosemekana

Zimesambaa baadhi ya picha katika mitandao ya kijamii kuwa Staa wa muziki kutoka Tanzania, Ambwene Allen Yessayah ‘AY’ amefunga ndoa na mpenzi wake anayefahamika kwa jina la Reheme au Remmy na sasa baada ya chumba cha haabari kilifanyika kazi hilo yapo machache ambayo yamegundulika na tumepata undani wa kilichoendelea katika shughuli hiyo iliyofanyika siku ya jana nchini Rwanda.

AY na Remmy wamekuwa katika mahusiano kama wachumba kwa muda mrefu sasa na kwa mujibu wa chanzo chetu(Mwenyeji na mdau mkubwa wa muziki wa nchini Rwanda) amesema kuwa, kilichofanyika siku ya jana kati ya AY na Remmy sio Ufungaji wa ndoa bali ni utoaji wa mahari ambao kwa lugha ya asili nchini humo inafahamika kama ‘Gusaba no Gukwa’ au kwa lugha ya kifaransa ‘DOTÊ’.

Sherehe hizo za utoaji mahari kawaida ufanyika nyumbani kwa mwanamke lakini kwa AY zimefanyika katika hotel ya Golden Tulip La Palisse iliyoko nje kidogo ya mji wa Kigali na wazazi wa wapenzi hao walikutana, wakapa nafasi ya kufurahia muunganiko huo wa watoto wao na kufahamiana Zaidi.

Hata hivyo zoezi hilo la utoaji mahari limeambatana na utambulisho wa mwanaume kwa wazazi wa mwanamke na sherehe hiyo haikuwa na mbwembe za umaarufu  mbali na kuwa watu maarufu waliopata mualiko. Walikuwepo miongoni mwa walioudhuria ni pamoja msanii Mwana FA, Mtangazaji B Dozen, MC na mwanamitindo kutoka Kenya, Fundi Frank, meneja wa msanii AY ‘Sallam SK a.k.a Mendez, mdau wa muziki na mtangazaji maarufu nchini humo Rwanda ‘Tidjara Dada Kabendera’Wengine wengi.

Comments

comments

You may also like ...