Header

Diamond bado hajajua Valentine wake atakuwa nani

Zikiwa zimebaki siku 2 kufikia siku ya wapendanao ijulikanayo kama ‘Valentine Day’ Mmiliki wa Lebo ya WCB Diamond Platnumz amtaja Valentine wake wa siku hiyo ambapo amedai itategemea na wapi itakapo mkuta siku hiyo.

Akizungumza na Dizzim Online Msanii huyo ambae kwa karibuni alipamba vichwa vya Habari baada ya kukatikiwa kiatu chake Mahakamani amesema Valentine wake atamjua pale ambapo itafika siku hiyo ya February 14 mwaka huu.

” Sasa itategemea itanikuta wapi siku hiyo kama itanikuta kwa mzazi mwenzangu basi atakuwa yeye lakini kama ikinikuta huku Tanzania basi Valentine wangu watakuwa ndugu zangu na marafiki zangu” Amesema Staa huyo.

Aidha Diamond amewaomba Watanzania waendelee kumpa support msanii mpya wa WCB Mbosso ili aweze kufika mbali zaidi kimuziki kama walivyoweza kufika wao.

Comments

comments

You may also like ...