Header

Beka Flavour akataa kufugwa kimapenzi, Aimba kwa msisitizo wa kula jasho lake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Bakari Katuti a.k.a Beka Flavour amekataa kila tabia ya maisha ya kimapenzi ya kuishia kupewa huduma za mahitaji yake na kusubiria aletewe kila kitu na mpenzi wake ‘Kibenteni’.

Staa huyo wa ngoma kama vile, Libebe, Sikinai na Sarafina, amesikia akiikataa hali hiyo ya kimahusiano kupitia wimbo wake mpya kwa jina ‘Kebenteni’ ambapo wimbo huo ameutoa sambamba na video ilioyoongozwa na Director Creator Pro.

Hata hivyo Audio ya wimbo huo imekamilishwa chini ya ushirikiano wa watayarishaji wawili ambao ni hit song producer wa wimbo wa Aiyola ya Harmonize, Maximaizer akiwa ameshirikiana na Producer mwenzake Mafia.

Comments

comments

You may also like ...