Header

Chemical amlambisha asali Producer Maxmizer mchana kweupe

Mrembo na mkali wa muziki wa Rapa kutoka Tanzania, Chemical amelegeza mkanda  wa alichobana kwa muda mrefu na tena kwa mara hii imekuwa ni mbele ya kamera kwa Mtayarishaji Maxmaizer ambapo imeonekana kuwa alishikwa vilivyo.

Chemical amekuwa ni mwenye kusimamia msimamo wake wa kuishi Single life kimahusiano mbali na kuwa wapo waliowahi kujitokeza kumhitaji ili wawe naye kimapenzi ambapo baada ya kuzungumzwa sana juu ya kuishi bila kuwa na mpenzi alifika hatua ya yeye kuweka wazi kuwa bado ni bikira kitu ambacho wachache walikiamini.

Kutoka katika video ya kolabo ya wimbo wake na Mwimbaji Beka Flavour kwa jina ‘Asali’, imetokea na kusamba kwa picha iliyomuonesha Chemical akikutanisha lips zake na lips za producer Maxmizer ambaye ni mtayarishaji wa wimbo huo na pia alisimama katika nafasi kama video king wa Video ya wimbo huo.

Hata hivyo tukio la namna hii kwa Chemical ni kwa mara ya pili kwakuwa mara ya kwanza alishakiri kuwa lips zake za lips za video king aliyetumika katika video ya wimbo wake wa ‘Am sorry Mama’ zilikutana kweli kweli na hayakuwa maigizo tu kama baadhi ya watu walivyodhani.

Comments

comments

You may also like ...