Header

Dicky Ability kuachia nyingine kutoka kwa Sheddy Clever, Autamani mkono wa Director Hansacana

 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Dickson Ramadhan a.k.a Dicky Ability ametangaza ujio mwingine ndani ya miezi mmoja ujao baada ya kuachia ‘Tamu Yangu’ iliyofanyika chini ya utayarishaji wa Sheddy Clever kutoka Burn Records ambapo video ya wimbo huo iliongozwa na Director Deo Abel.

Akipiga stori na Dizzim Online, Dicky amesema kuwa kwa sasa ameshafikia maamuzi ya ngoma ipi itoke kati ya mbili Ilizobaki na kugusia kuwa ipo iliyopewa kipaumbele na Uongozi ambayo utayari wake pia umekamilika chini ya Sheddy Clever.

“Mara hii siwaachii nafasi hata kidogo. yaani ngoma zipo kabao, kolabo za wasanii wa ndani na nje ya nchi, lakini ipo ambayo Sheddy kagonga na Management naona kama ndo inaitolea macho sana. Kama unavyojua mambo ya uongozi bana…kikubwa mashabiki wajue kazi kali zipo na mwezi ujao naachia kitu kingine” Amesema Dicky Ability.

Hata hivyo Dicky hakuweka bayana video ya kazi ipi itakayotoka na itakuwa imeongozwa na Director yupi lakini amesema kuwa kati ya nyimbo zilizokamilika, ipo ambayo anatamani uongozi usimamie ili wimbo huo uongozwe na Director Hanscana.

“Kuhusu video siwezi kusema sana lakini pia video za baadhi za kazi zimeshakamilika na sijajua ipi na ni ya Director yupi itatoka lakini ipo ambayo nimezungumza na Management yangu ili Hasacana atishe kwakuwa Hans ni katika ya madirector wakali Bongo ninaowakubali kinoma noma” Ameongeza.

Dicky kwa sasa anafanya kazi chini ya mkataba na lebo ya muziki inayosimamia kila hatua ya muziki inayofahamika kwa jina ‘Moo Entertainment’ inayopatikana nchini Tanzania.

Itazame Tamu Yangu ya Dicky Ability.

Comments

comments

You may also like ...