Header

“Nikikukubalia Rushwa ya ngono jiandae kudhalilika”;- Witness

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Witness a.k.a Kibonge Mwepesi, ametoa sababu ya yeye kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagran wenye maneno makali yaliyoashiria kuchoshwa na baadhi ya watangazi na waandaaji wa vipindi kwenye Media tofauti tofauti  ambazo hakutaka kabisa kuzitaja.

Akizungumza na Dizzim Online Msanii huyo ambae pia ni mfanya biashara wa bidhaa mbali mbali amesema kuwa anachukizwa  sana na rushwa za ngono zinazo endelea kwenye media tofauti tofauti ambazo zinaangaliwa sana kuliko kipaji cha msanii.

“Nimeamua kuandika vile kutokana na rushwa za ngono zinazoendelea kwenye Radio station na TV Station, producer na djs  vimekuwa vikiendelea kwa muda mrefu tangu nilipoanza muziki kama miaka 20  hivi sasa ambayo nimekuwa nikivikwepa  na kupingana navyo  vitu kama hivyo na mimi siwezi kutoka na watu kama vigogo au viongozi wa Serikali au mtu yeyote mwenye wadhifa wake kwamaana kwamba mimi sitoki na mtu kwasababu nipate kitu flani kwasababu najua kitu nilichokuwa nacho kina thamani kubwa sana ambapo kama watu wakiamua kukithamini  na kukiheshimu basi nitafikia mbali zaidi” Alisisitiza msanii Wetness.

Aidha ameongeza na kusema kuwa endapo atamkubali yeyote atakae muomba Rushwa ya ngono basi ajue kuwa huko atakapoenda kuonana nae basi atakuwa na camera pamoja na vyombo vya dola.

Comments

comments

You may also like ...