Header

Saida Karoli na Hanson Baliruno waachia kolabo zao kwa kupokezana

Mkongwe wa muziki wa asili na tamaduni ya kabila la Magharibi mwa Tanzania, Saida Karoli ameachia wimbo mpya akiwa ameshirikiana na Mwimbaji wa kiume wa nyimbo za aina yake anayefanya vizuri kutoka nchini Uganda ‘Hanson Baliruno’ na ipo nyingine ambayo imetoka audio kutoka kwa Hanson akiwa amemshirikisha Saida.

Saida na Hanson wamemua kuachia kazi zao za pamoja na hii ambayo Saida amemshirikisha Hanson kwa jina ‘Akatambala’ imetoka sambamba na video iliyoongozwa na Director kutoka nchini Uganda kwa jina Ian Akankwasa a.k.a Sasha Bybez.

Hanson Baliruno ambaye anafanya vizuri na wimbo wake kwa jina ‘Kandanda’ kwa sasa, naye ameachia wimbo wake mpya ambao amemshirikisha Saida unaokwenda kwa jina ‘Oburo’.

 

Comments

comments

You may also like ...