Header

Willy Paul baada ya Ushawishi, kudonosha Malingo

Msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya, Wilson Abubakar Radido a.k.a Willy Paul ameweka picha ya kava ya wimbo wake mtadaoni na kutangaza kuwa video ya wimbo wake huo unaotegemewa kwa jina ‘Malingo’ inatoka hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Willy Paul ameweka kava ya wimbo huo uliotayarishwa chini ya studio za Soldido Records ambapo kwa mujibu wa maudhui ya kava ya wimbo imehisiwa kuwa utazungumzia hali ya kumjali mtoto wa kike kwa namna ambayo baadhi ya walitoa maoni walichangia kuwa unaweza kuwa ni wimbo wa mapenzi.

Hata hivyo ujio huu kutoka kwa Willy Paul utatoka kama kazi yake ya kwanza kwa mwaka wa 2018 na ni ujio utakao toka baada ya wimbo wake wa ‘Tempted’ uliotoka mwishoni mwa jana chini ya utayarishaji wa Studio hizo hizo za Soldido Records.

 

Comments

comments

You may also like ...