Header

Chemical ashindwa kificha kilichomkaba kooni kwa Maxmaizer

Hakika mapenzi yanaonekana kuwa yameanza kupeperushwa mubashara kati ya msanii wa muziki wa rapa na Matayarishaji wa muziki kutoka Tanzania. Baada ya kubainika kuwa rapa wa kike Chemical amelegeza hisia zake kwa Mtayarishaji Maxmaizer, Chemical amesisitiza kuwa anachokipata kutoka kwa mtayarishaji huyo ni Asali.

Ikizingatiwa kuwa wimbo mpya wa Chemical unakwenda kwa jina la Asali, kwa mujibu wa alichokiandika sambamba na picha yake aliyopost kwenye mtandao wa Instagram akiwa katika busu lenye hisia nzito na Maxmaizer, imeonekana kuwa hali ya upendo inaweza kuwa imemzidia na kwa sasa hawezi kuficha tena.

Hata hivyo kama hili la Chemical na Maxmaizer  halitaishia katika kile kilichoonekana kwenye wimbo wa Asali basi Maxmaizer atakuwa ni mwanaume mwenye bahati ya mtende kwani inaweza kuaminika kuwa ni kwa mara ya kwanza anabamkabidhi mwanaume moyo wake ili wafurahie Penzi tangu athibitishe kuwa yeye bado ni bikra Mwaka jana.

Comments

comments

You may also like ...