Header

Huyu ndiye Valentine wa Snura.

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Snura Mushi a.k.a Snu Sex ametolea ufafanuzi juu ya picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha yeye na Mwanaume anaejulikana kwa jina la Muni.

Akipiga story na Dizzim Online mkali huyo anayetamba na kibao cha Moyo Niache aliomshirikisha msanii Aslay, amesema kila kitu kilichoonekana kwenye mitandao ya kijamii ni kweli hakuna kitu cha uongo hata kimoja.

“Huyi kaka ni kweli mpenzi wangu na sina muda mrefu toka nilipofanya maamuzi ya kuwa nae mwanzoni alikuwa mshikaji wangu tu japokuwa watu wengi walihisi tuna mahusiano na niliwakatilia kwakuwa ndio ukweli uliopo kwa kipindi kile  kwamba hatukuwa wapenzi lakini kwa sasahivi ndio mpenzio wangu na nina mpenda kwa dhati na ndio Valentine wangu” amesema staa huyu.

Aidha aliongeza na kusema Mwanaume huyo ndiye Mtu  pekee aliyeokoa maisha yake kwa kiasi kikubwa sana hivyo hana budi kumpenda kwa dhati.

Comments

comments

You may also like ...