Header

Nyashinski arusha mkuki wa Mapenzi kwa Mashabiki ‘Valentine’s Day’

Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Nyamari Ongegu ‘Nyashski’ amewapa mashabiki zawadi ya wimbo wenye maudhui ya kimapenzi katika siku ya wengi kuonesha mapenzi kwa wawapendao na kuwajali ‘Valentine’s Day’.

Staa huyo wa ngoma ya ‘Malaika’, ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Bebi Bebi’ iliyotayarishwa chini ya Studio za Ogopa Djs huku video ikiongozwa na Director Tosh Gitonga kutoka katika kampuni ya  Blink Production Ltd ya nchini Kenya.

Hata hivyo Staa huyo wa zamani wa kundi la Kreptomania la nchini Kenya, ni mwaka sasa tangu rapa huyu arudi rasmi katika muziki kama Solo Artist na wimbo huu unakamilisha idadi ya ngoma sita(6) baada yake ya mwisho ‘Hayawani’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana.

Itazame Video ya wimbo huo mpya.

Comments

comments

You may also like ...